Friday, May 31, 2013

Legendaries wamechoshwa na unyonyaji wa Clouds....

Ni kwa kiasi kikubwa mziki wa bongo unaumiza,
na wasanii wengi wanakaa kimya wakihofia endapo tu watasema ukweli na kudai haki zao watakosa hata kile kidogo wakipatacho ingawa wananyonywa, hali ambayo imepelekea wengi wao kuishi maisha duni na ya umaskini wa hali ya juu.
P funk (majani) ameamua kusema ukweli na kuamua kujitoa na wanyonyaji hao (clouds fm) kwani wao ndio wanaoungamiza mziki wa bongo,wasanii na vipaji.
katika interview ambayo aliifanya, majani aliwapa makavu na kutoa tamko kua hatapenda kuona clouds wakipiga nyimbo zake(marufuku) zilizotengenezwa bongo record na za wasanii wote wa bongo record.
Hatua hii imenifurahisha na kunipa hamasa kua huenda muziki wetu (na hasa Hip Hop) utanusurika kutoka kwa hawa wanyonyaji, na hali itarudi kama zamani.
Hapo nyuma alianza Mr II (Sugu) alipoanzisha harakati hizo, akaungana na vinega na harakati ikapewa jina la antivirus, lengo na nia kuu ikiwa ni kuondoa unyonyaji unaofanywa na clouds fm wakiongozwa na ruge mutahaba.
Lady jaydee naye akafuatia na kuwapa makavu, lakini baadhi ya watu wakaanza kusema kua, wanatumiwa na baadhi ya watu kuweka vugu vugu la choko choko,
Je, majani naye (P funk) anatumiwa??

Tafakari na chukua hatua ili tuunusuru Muziki wetu na hasa Hip Hop.
Mabadiliko ni wewe!!!

Okoa HIP HOP!