Monday, September 2, 2013

Shy town: hizi ni harakati na matunda yenu....


         Ilikua ni ngumu sana kipindi harakati zinaanza, watu wengine waliona ni kama masikhara pale walipoambiwa kua wasanii wote wa shinyanga waungane na wafanye tamasha ambalo halitakua na kiingilio (Bure kabisaa) kwa watu wote, lengo na nia ni kusambaza ujumbe na vipaji vilivyosheheni shinyanga (Shy town).
    Wengine walichukulia kama mzaha flani, na wengine wakiitikia kwa mdomo tu lakini kutimiza ikawa ni story ndefu, lakini hilo halikunivunja moyo wala kunikatisha tamaa katika mipango yangu ya harakati katika sehemu iliyonikuza na kunilea, na ninaapa kamwe siwezi kurudi nyuma wala kukatishwa tamaa na wasaliti ambao upeo wao ni finyu sana.

 "Unapoamua kufanya harakati za mapinduzi ukubali kuumia, kuteseka, na hata kudharaulika maana watu hawaelewi thamani ya malengo na mipango iliyopo mpaka waone matunda yake ndio husadiki" Big.com.

 Big.com(The Black Incredible Gangster comrade) ni mwanaharakati aliye katika misingi ya Hip Hop, ambaye alikaa chini, yeye pamoja na Mack fe, Jereone kwa pamoja sana na steve kanyeph (Mwanapori), na kuamua kuandaa jambo litakaloweka vijana na vipaji kutoka shy town sehemu moja, na hasa Hip Hop. Harakati zilianza mtaa kwa mtaa, Mguu kwa mguu bila ya kua na udhamini wowote, mpaka siku ilipotimia ambapo show ilifanyika katika ukumbi wa ry misanga pasipo kua na kiingilio chochote. show ilijumuisha waimbaji pia, michano ya Hip Hop na battles za maana kutoka kwa machizi wa kitaa. Tamasha hilo ni muendelezo wa matamashha ambayo yamepangwa kua yakifanyika kila mwaka, lengo kuu na nia ni kuonyesha vipaji vyetu na kusaka heshima kwa jamii zinazotuzunguka.
      "kwa nini msanii akitokea nje ya shy town anaonekana anajua sana na mzawa adharaulike ile hali vipaji vipo vya kutosha?" alihoji Big.com.

  Nahitaji siku moja muziki unilipe (Utulipe) hata kama sio kwa pesa, heshima ni kitu muhimu zaidi kwa mtaa...

Viva shy town...
Viva shy town Music...
Viva Big.com!

No comments:

Post a Comment

type in here..