Jina la juliani, na nyota yake ilianza kung'aa pale alipotoka na "bahasha ya Okampo" akitoa hisia zake hali ilivyo nchini Kenya kuhusu masuala ya uongozi na siasa kiujumla, haki na uhuru wa raia wa Kenya.
Kama umepata kusikia na kuyafuatilia mashairi yake, Juliani huongelea sana mambo ya siasa hasa za Kenya, akitoa taswira na picha halisi kuhusu vuongozi na maovu yanayofanywa na viongozi hao.
Kwa upande wake yeye anaiongelea kenya, lakini katika hali halisi, haya ni matatizo ya waafrika na hasa tanzania ambayo yanatukabili.
Hip Hop ni kuongelea ukweli wa mambo na matatizo ya jamii tunazoishi na kutuzunguka, na hili linanifanya nipende sana kumsikiliza juliani kwa sababu anasimamia ukweli huo na nguzo.
Kibao Chake "Utawala" ni wimbo unaosisimua na kuvuta hisia, kwani ameongelea ukweli na hali halisi ya viongozi, uongozi wetu, makosa tunayofanya sisi na yale yanayofanywa na viongozi wasio na weledi(wanasiasa feki).
"niko njaa hata siwezi karanga,
hohe haaaheee, shaghalabaghala,
niko tayari, kulipa gharaama,
sitosimama maovu yakitawala..."
hayo ni baadhi ya maneno yanayopatikana katika wimbo huo "Utawala".
usikilize hapa..
No comments:
Post a Comment
type in here..