Saturday, July 27, 2013

He is the Game, He do the Game.....



Hivi, ulishawahi kujiuliza album nzima ya msanii yeyote ina stanza(bars) ngapi?
wimbo mmoja unakua na stanza ngapi?

kwa hesabu za haraka haraka ni kwamba, nyimbo nyingi za hip hop(za sasa), kila ubeti unakua na stanza 16(16 bars),
na kwa hesabu za haraka haraka wimbo mmoja unakua na stanza 48 kwa anayetunga beti 3(3 verses), na 32 kwa atungaye
beti 2(2 verses).
Hapa kwa hesabu za jumla, kama album ina nyimbo 10, jamaa anakua na stanza 480 kwa anayetunga verse 3 na 320 kwa anayetunga verse 2,
kwa hyo tukiweka mlinganyo unakuta stanza zinachezea kati ya 300 na 400.

Je, umepata kuzisikiliza au kuzisoma stanza 400(400 bars) za THe GaMe??
kwa ufupi, jamaa kaimba mashairi ya album nzima ndani ya wimbo mmoja, ambapo mashairi hayo yangeandikiwa wimbo mmoja mmoja wenye stanza 32 kila mmoja ungepata nyimbo zaidi ya 12....

hii ni changamoto sana kwa watu wanaofanya Hip Hop halisi, nikimaanisha wale wenye uzalendo na uchungu na mziki na utamaduni wetu wa hip Hop.

Nimeandika habari hii kutokana na uchungu nnaoupata kutokana na jinsi RAPPERS wa sasa wanaotaka kujifanya MC's, wakiweza kutumia beat ya Hip Hop bas wanajiita nao ni wana Hip Hop mahiri na wanaotumia mda wao kutunga sana mashairi....
nakupa task rahisi sana, wewe kama mwana Hip Hop, unaweza kuimba mashairi yote hayo ndani ya wimbo mmoja bila kupumzika?
Je,unaweza kuyakumbuka mashairi hayo?
Hip hip inahitaji kuitolea muda wa kutosha ili kuifikisha sehemu inayistahili....

keep it gangster....
Keep Hip Hop alive...
Let the good music live...

Big.com

No comments:

Post a Comment

type in here..