Saturday, October 12, 2013

Monday, September 2, 2013

Shy town: hizi ni harakati na matunda yenu....


         Ilikua ni ngumu sana kipindi harakati zinaanza, watu wengine waliona ni kama masikhara pale walipoambiwa kua wasanii wote wa shinyanga waungane na wafanye tamasha ambalo halitakua na kiingilio (Bure kabisaa) kwa watu wote, lengo na nia ni kusambaza ujumbe na vipaji vilivyosheheni shinyanga (Shy town).
    Wengine walichukulia kama mzaha flani, na wengine wakiitikia kwa mdomo tu lakini kutimiza ikawa ni story ndefu, lakini hilo halikunivunja moyo wala kunikatisha tamaa katika mipango yangu ya harakati katika sehemu iliyonikuza na kunilea, na ninaapa kamwe siwezi kurudi nyuma wala kukatishwa tamaa na wasaliti ambao upeo wao ni finyu sana.

 "Unapoamua kufanya harakati za mapinduzi ukubali kuumia, kuteseka, na hata kudharaulika maana watu hawaelewi thamani ya malengo na mipango iliyopo mpaka waone matunda yake ndio husadiki" Big.com.

 Big.com(The Black Incredible Gangster comrade) ni mwanaharakati aliye katika misingi ya Hip Hop, ambaye alikaa chini, yeye pamoja na Mack fe, Jereone kwa pamoja sana na steve kanyeph (Mwanapori), na kuamua kuandaa jambo litakaloweka vijana na vipaji kutoka shy town sehemu moja, na hasa Hip Hop. Harakati zilianza mtaa kwa mtaa, Mguu kwa mguu bila ya kua na udhamini wowote, mpaka siku ilipotimia ambapo show ilifanyika katika ukumbi wa ry misanga pasipo kua na kiingilio chochote. show ilijumuisha waimbaji pia, michano ya Hip Hop na battles za maana kutoka kwa machizi wa kitaa. Tamasha hilo ni muendelezo wa matamashha ambayo yamepangwa kua yakifanyika kila mwaka, lengo kuu na nia ni kuonyesha vipaji vyetu na kusaka heshima kwa jamii zinazotuzunguka.
      "kwa nini msanii akitokea nje ya shy town anaonekana anajua sana na mzawa adharaulike ile hali vipaji vipo vya kutosha?" alihoji Big.com.

  Nahitaji siku moja muziki unilipe (Utulipe) hata kama sio kwa pesa, heshima ni kitu muhimu zaidi kwa mtaa...

Viva shy town...
Viva shy town Music...
Viva Big.com!

Tuesday, August 13, 2013

Juliani: the illest Kenyan Hip Hop Mc...

Jina la Juliani ni geni sana masikioni kwa watu wengi ambao hawafuatilii muziki kiundani, lakini kwa wale wenye mapenzi ya kweli na muziki na wanaosupport mziki wa kweli, Juliani si jina geni kwao, na ni mmoja kati ya wanaharakati na wana Hip Hop mahiri waliosalia nchini Kenya, Africa na Duniani kwa ujumla.




Jina la juliani, na nyota yake ilianza kung'aa pale alipotoka na "bahasha ya Okampo"  akitoa hisia zake hali ilivyo nchini Kenya kuhusu masuala ya uongozi na siasa kiujumla, haki na uhuru wa raia wa Kenya.

Kama umepata kusikia na kuyafuatilia mashairi yake, Juliani huongelea sana mambo ya siasa hasa za Kenya, akitoa taswira na picha halisi kuhusu vuongozi na maovu yanayofanywa na viongozi hao.
Kwa upande wake yeye anaiongelea kenya, lakini katika hali halisi, haya ni matatizo ya waafrika na hasa tanzania ambayo yanatukabili.

Hip Hop ni kuongelea ukweli wa  mambo na matatizo ya jamii tunazoishi na kutuzunguka, na hili linanifanya nipende sana kumsikiliza juliani kwa sababu anasimamia ukweli huo na nguzo.



Kibao Chake "Utawala" ni wimbo unaosisimua na kuvuta hisia, kwani ameongelea ukweli na hali halisi ya viongozi, uongozi wetu, makosa tunayofanya sisi na yale yanayofanywa na viongozi wasio na weledi(wanasiasa feki).



"niko njaa hata siwezi karanga, 
  hohe haaaheee, shaghalabaghala,
  niko tayari, kulipa gharaama,
  sitosimama maovu yakitawala..."
hayo ni baadhi ya maneno yanayopatikana katika wimbo huo "Utawala".

usikilize hapa..




Monday, July 29, 2013

The best speech of all the time...



Have you ever heard of him?
Have you ever seen him?
They call him Immortal Technique, the true nigga who sacrificed himself to defend the poor...
He never afraid to speak and talk when it comes the matter of truth....

Will you defend the truth?
will you stand for your rights?

Saturday, July 27, 2013

He is the Game, He do the Game.....



Hivi, ulishawahi kujiuliza album nzima ya msanii yeyote ina stanza(bars) ngapi?
wimbo mmoja unakua na stanza ngapi?

kwa hesabu za haraka haraka ni kwamba, nyimbo nyingi za hip hop(za sasa), kila ubeti unakua na stanza 16(16 bars),
na kwa hesabu za haraka haraka wimbo mmoja unakua na stanza 48 kwa anayetunga beti 3(3 verses), na 32 kwa atungaye
beti 2(2 verses).
Hapa kwa hesabu za jumla, kama album ina nyimbo 10, jamaa anakua na stanza 480 kwa anayetunga verse 3 na 320 kwa anayetunga verse 2,
kwa hyo tukiweka mlinganyo unakuta stanza zinachezea kati ya 300 na 400.

Je, umepata kuzisikiliza au kuzisoma stanza 400(400 bars) za THe GaMe??
kwa ufupi, jamaa kaimba mashairi ya album nzima ndani ya wimbo mmoja, ambapo mashairi hayo yangeandikiwa wimbo mmoja mmoja wenye stanza 32 kila mmoja ungepata nyimbo zaidi ya 12....

hii ni changamoto sana kwa watu wanaofanya Hip Hop halisi, nikimaanisha wale wenye uzalendo na uchungu na mziki na utamaduni wetu wa hip Hop.

Nimeandika habari hii kutokana na uchungu nnaoupata kutokana na jinsi RAPPERS wa sasa wanaotaka kujifanya MC's, wakiweza kutumia beat ya Hip Hop bas wanajiita nao ni wana Hip Hop mahiri na wanaotumia mda wao kutunga sana mashairi....
nakupa task rahisi sana, wewe kama mwana Hip Hop, unaweza kuimba mashairi yote hayo ndani ya wimbo mmoja bila kupumzika?
Je,unaweza kuyakumbuka mashairi hayo?
Hip hip inahitaji kuitolea muda wa kutosha ili kuifikisha sehemu inayistahili....

keep it gangster....
Keep Hip Hop alive...
Let the good music live...

Big.com

Friday, July 26, 2013

i call real Hip Hop



Cheki jinsi video ilivyosawiri mazingira halisi ya hip hop,
kila mtu ametokea location yake,
location zinazosisimua na kuvutia...

Hip Hop for life...

Friday, May 31, 2013

Legendaries wamechoshwa na unyonyaji wa Clouds....

Ni kwa kiasi kikubwa mziki wa bongo unaumiza,
na wasanii wengi wanakaa kimya wakihofia endapo tu watasema ukweli na kudai haki zao watakosa hata kile kidogo wakipatacho ingawa wananyonywa, hali ambayo imepelekea wengi wao kuishi maisha duni na ya umaskini wa hali ya juu.
P funk (majani) ameamua kusema ukweli na kuamua kujitoa na wanyonyaji hao (clouds fm) kwani wao ndio wanaoungamiza mziki wa bongo,wasanii na vipaji.
katika interview ambayo aliifanya, majani aliwapa makavu na kutoa tamko kua hatapenda kuona clouds wakipiga nyimbo zake(marufuku) zilizotengenezwa bongo record na za wasanii wote wa bongo record.
Hatua hii imenifurahisha na kunipa hamasa kua huenda muziki wetu (na hasa Hip Hop) utanusurika kutoka kwa hawa wanyonyaji, na hali itarudi kama zamani.
Hapo nyuma alianza Mr II (Sugu) alipoanzisha harakati hizo, akaungana na vinega na harakati ikapewa jina la antivirus, lengo na nia kuu ikiwa ni kuondoa unyonyaji unaofanywa na clouds fm wakiongozwa na ruge mutahaba.
Lady jaydee naye akafuatia na kuwapa makavu, lakini baadhi ya watu wakaanza kusema kua, wanatumiwa na baadhi ya watu kuweka vugu vugu la choko choko,
Je, majani naye (P funk) anatumiwa??

Tafakari na chukua hatua ili tuunusuru Muziki wetu na hasa Hip Hop.
Mabadiliko ni wewe!!!

Okoa HIP HOP!

Wednesday, April 24, 2013

KRS One -tribute to NAS

Muungano huu ni kutokana na pale NAS alipotoa kibao "Hip Hop is dead", akiwa anataka kuelezea mapungufu yaliyopo sasa katika Hip Hop.

KRS One naye alijibu kwa kusema "Hip Hop lives" akitaka kuelezea ni jinsi gani Hip HOP inaendelea Kuiteka dunia na uwepo wake katika Hii Sayari.

Baada  ya kuonekana kama kuna bifu flani, ndipo walipoungana na kuunganisha mawazo yao na kutoka na ngoma "tribute to Nas".
Pata kuisikiliza usikie ni kipi walichokisema.

Friday, April 19, 2013

G-san katika BET awards ... Mtanzania pekee aliyepata nafasi BET cypher

mtanzania pekee aliyetuwakilisha katika tuzo za BET akiwa pamoja na KRS-One, Nipsey hustle pamoja na Wale.

Hip Hop lives in Tanzania

Tuesday, April 9, 2013

Happy BirthDate Big.com...

anaitwa
"Black Incredible Gangster comrade..." au wengi walivyozoea
Big.com, mwanaharakati.....
bofya linki hii upate kumjua kiundani

The Black Incredible Gangster comrade(Big.com)

Sunday, April 7, 2013

Shy town Hip Hop: the movement....















hivi ndivyo vijana wa shy town wanavyofanya katika mtaa katika show zinazofanyika bure kila mwaka....


join the revolution....

Thursday, April 4, 2013

Mr II ...

 mmeutoa mbali muziki....
acha mle matunda.

Immortal Technique Announces Rebel Armz Album & "The Martyr 2"




Exclusive: Immortal Technique also updates "The Middle Passage" and explains delays.


Technique revealed information about his next few projects and provided an exclusive regarding a Rebel Armz album.


"I've got people playing instruments on this mothafucka," Technique said of his highly anticipated album, The Middle Passage. Technique continued by saying that he had to scrap two songs from the project recently because of issues clearing samples.


"I really wanted to go all out and have an organic sound but it's still Hip Hop. This doesn't sound like an Opera album or some crazy shit like that. We didn't go off the deep end but technically, I had to scrap two [songs]. What came out of that was also the idea that if 'The Martyr' was so successful - because we did over a million downloads for it - if 'The Martyr' was so successful, we're gonna have to have a 'Martyr 2' now. That unreleased song is gonna go on 'The Martyr 2.'"


Next, Technique shared that he has plans to release a collaborative project with Rebel Armz, a group of emcees that includes Poison Pen and Diabolic.


"I'll be able to put out The Middle Passage, 'The Martyr [2]' and me, [Poison] Pen, Diabolic and the rest of the crew have been kicking the idea around a lot about doing a Rebel Armz album and I think it's overdue. So I'm gonna say, since y'all like exclusives, that we are definitely gonna do it. This is the first time I'm saying it. The Rebel Armz album [with] Immortal Technique and the whole fuckin' squad is gonna happen. It's going down."


The Middle Passage has been delayed for several years. In 2010, Technique said he was working on the album, which was to be a "conceptual" project. By 2011, Technique explained that he hoped to release the album in the first quarter of the following year. “[It’s about] halfway done," he explained then. In that same year, Technique released "The Martyr" to critical praise and over a million downloads online. The Rebel Armz consists of various emcees including Technique, Chino XL, Swave Sevah andAkir.

Saturday, March 30, 2013

Friday, March 29, 2013

Did you hear this?


The lyrics deal with the idea of hip-hop's death as artistically viable music, as explained below:
Everybody sounds the same, commercialize the game
Reminiscin' when it wasn't all business
It forgot where it started
So we all gather here for the dearly departed
Nas clearly decries the idea that hip hop has gone the way of commercialization, pledging to stay true to its origins, as in the last line of verse 1, where Nas mentions MC Shan and MC Ren, by saying So nigga, who's your top ten, is it MC Shan is it MC Ren.
Nas also mentions NBA commissioner David Stern.

Thursday, March 7, 2013

Sunday, January 27, 2013

tanzania Top 15 Mc's

Orodha ya wana Hip Hop mahiri Tanzania (The top 15 best hip hop Mc's and crews in Tanzania)

tukisema hip hop Tanzania,
tunawaongelea watu hawa.

01. Kwanza Unit
02. Mr II a.k.a Sugu
03. Hard Blasters Crew (H.B.C)
04. X-Plastaz
05. Gangwe Mobb
06. Professor Jay a.k.a daddy
07. Juma Nature a.k.a kiroboto
08. Sollo Thang Ulamaa a.k.a mtravellah
09. Dollasoul a.k.a Balozi
10. Daz Nundaz
11. East Coast team
12. Wateule
13. Afande Selle
14. Fid Q
15. Watengwa

Kama ukifanya uchunguzi kuanzia game yetu ya Bongo flavour inaanza, mziki uliokumbwa na misukosuko mingi na kupingwa a wazee kabla haujafanikiwa, utagundua kua list iliyo hapo juu ni watu waliohamasisha na, kupigania na kuhakikisha mziki wetu unasimama na kupata jina.
"Nilimshawishi baba'ko ili akuruhusu uimbe" ni moja kati ya mstari kutoka kwa Proffessor J, akiwa na maana kua, album yake ya mwanzo ya machozi,jasho na damu iligeuza fikra na taswira za wazee waliokua wakiona kua mziki ni uhuni hivyo kuanza kuamini kua ni vipaji na ni ajira pia.

kuna watu wataibuka sasa hivi na kukwambia kua wasanii mahiri tanzania ni kama Diamond, Ommy Dimpoz, na wengine wanaopenda kuimba na kusifia mapenzi tu, bila kujua na kukumbuka ni wapi mziki ulianzia na ni nani amefanya mpaka sasa game inaheshimika.

tutabishana sana lakini hawa jamaa walifanya na wanafanya mziki kweli, hata leo hii zikipigwa ngoma za zamani na za sasa, masikio yote yatahamia na kung'ang'ania za zamani kwa sababu kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza.
hebu angalia jinsi walivyojitoa kuhangaikia licha ya kudharauliwa na kuonekana wajinga,
hapa ni mr II katika viwanja vya mnazi mmoja



takwimu hizi ni kutokana na uchunguzi niliofanya tangu game linaanza mpaka sasa lilipofikia,
Na mpangilio ni kutokana na takwimu zangu na si vinginevyo.

Hip Hop for life!!


Saturday, January 26, 2013

they call him immortal technique...











 i call him the best rapper alive,
the illest rapper i've ever seen!!

let's us speak to our minds.
Revolutionaryyy...